Monday, 9 November 2015

WANAJESHI WA ISRAEL WAMUUA MWANAMKE MPALESTINA


Mwanamke mmoja Mpalestina ameuawa na vikosi vya utawala haramu wa Israel katika kituo cha upekuzi barabarani huko katika Ukingo wa Magharibi na hivyo kupelekea idadi ya Wapalestina waliouawa na Wazayuni katika kipindi cha siku 40 zilizopita kuwa 80. Duru za Palestina zimedokeza kuwa mwanamke huyo amepigwa risasi na kuuawa shahidi leo katika eneo la Qalqailya. Wanajeshi wa Israel wamedai kuwa mwanamke huyo aliwashambulia kwa kisu.

Wizara ya Afya ya Palestina inasema Wapalestina 80 wakiwemo wanawake wanne na watoto 17 wameuawa na wanajeshi wa utawala wa Israel tokea mwanzo wa mwezi wa Oktoba.

Aghalabu ya Wapalestina wameuawa mashariki mwa Quds Tukufu (Jerusalem), Ramallah na al Khalil (Hebron).

Machafuko ya sasa Palestina inayokaliwa kwa mabavu yalianza kutokana na hatua ya utawala haramu wa Israel kuweka vizingiti kwa Wapalestina Waislamu kuingia katika Msikiti wa Al Aqsa. Israel inatekeleza njama za kuuyahudisha mji wa Quds na kuubomoa Msikiti wa Al Aqsa ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu.

No comments:

Post a Comment