Monday, 9 November 2015

WANAJESHI WA ISRAEL WAMUUA MWANAMKE MPALESTINA


Mwanamke mmoja Mpalestina ameuawa na vikosi vya utawala haramu wa Israel katika kituo cha upekuzi barabarani huko katika Ukingo wa Magharibi na hivyo kupelekea idadi ya Wapalestina waliouawa na Wazayuni katika kipindi cha siku 40 zilizopita kuwa 80. Duru za Palestina zimedokeza kuwa mwanamke huyo amepigwa risasi na kuuawa shahidi leo katika eneo la Qalqailya.

MAGUFULI ABADILI UONGOZI MUHIMBILI

 
Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli leo amefanya ziara nyingine ya kushtukiza, wakati huu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kufanyia mabadiliko usimamizi wa hospitali hiyo.Kiongozi huyo mpya amesikitishwa na kuhuzunishwa na hali ya huduma kwa wagonjwa hususan wanaolala chini, kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu.

NGOMA AFRICA BAND AKA FFU WAKIENDELEA KUDATISHA UGHAIBUNI WAFANYA KWELI JIJINI BREMEN


Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU-ughaibuni inayoongozwa na Kamanda Ras Makunja juzi jumamosi ya 7 November 2015 walifanikiwa tena kwa mara nyingine kukonga nyoyo za washabiki mjini Bremen Ujerumani katika onyesho la kusherekea miaka 10 ya Pan African Organisation